Tuesday, 19 August 2014

Tata Martino ataja kikosi cha Argentina kuivaa germany



Kocha aliyepata kuifundisha klabu ya Barcelona ya nchini Hispania Gerardo Martino ametangaza kikosi chake cha taifa cha argentina kitakachocheza na ujeruman katika mechi ya kirafiki katika mji wa Dusseldorf.


Kocha aliyepata kuifundisha klabu ya Barcelona ya nchini Hispania Gerardo Martino ametangaza kikosi chake cha taifa cha argentina kitakachocheza na ujeruman katika mechi ya kirafiki katika mji wa Dusseldorf.
 

 Gerlado martino kocha mpya wa timu ya taifa ya Argentina

 
Katika kikosi hicho hakuna mabadiliko sana kutoka katika kikosi alichokuwa nacho Alejandro Sabella katika mashindano ya kombe la dunia brazil mwezi june hadi july mwaka huu,isipokuwa wachezaji watatu pekee ndio wameachwa nje ambapo wachezaji hao ni Fernando Gago, Agustin Orion na Maxi Rodriguez.

Katika hatua hiyo ni kwamba martino ataweza kuongeza wachezaji wengine watatu katika mechi nyingine inayotarajiwa kuchezwa September 3 kutokana na kalenda ya FIFA kwa kuangalia hasa wale walio nje ya kwa sasa atakitegemea kikosi hicho alichokichagua.

Kikosi alichokichagua: Sergio Romero (Sampdoria), Mariano Andujar (Napoli); Pablo Zabaleta (Manchester City), Federico Fernandez (Napoli), Ezequiel Garay (Zenit St Petersburg), Marcos Rojo (Manchester United), Hugo Campagnaro (Inter Milan), Martin Demichelis (Manchester City), Jose Basanta (Fiorentina); Javier Mascherano (Barcelona), Lucas Biglia (Lazio), Ricardo Alvarez (Inter Milan), Augusto Fernandez (Celta Vigo), Angel Di Maria (Real Madrid), Enzo Perez (Benfica); Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Napoli), Sergio Aguero (Manchester City), Rodrigo Palacio (Inter Milan), Ezequiel Lavezzi (Paris Saint-Germain).

No comments:

Post a Comment