Tuesday, 19 August 2014

ILI KUBORESHA SOKA TANZANIA ,KOZI YA MAKOCHA KUFANYIKA SEPTEMBA 4 JIJINI DAR ES SALAAM


KOZI ya ukocha wa Leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) inatarajiwa kufanyika mara ya kwanza nchini,katika jiji la Dar es Salaam kuanzia Septemba 4 mwaka huu.
Mkufunzi wa kozi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume atatoka CAF, na itamalizika Septemba 8 mwaka huu wakati ada ya ushiriki ni sh. 300,000.

Washiriki wa kozi hiyo ni wale wenye leseni B ya ukocha ya CAF na  Fomu kwa ajili ya ushiriki wa kozi hiyo zinapatikana kwenye ofisi za TFF na tovuti ya TFF.
 Wakati huo huo: Makocha wa kombaini za mikoa zitakazoshiriki Copa Coca-Cola mwaka 2014 pamoja na waamuzi vijana wa michuano hiyo watashiriki kozi ya ukocha na uamuzi itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu.

Kozi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa itakayochezwa Septemba mwaka huu.

Waamuzi vijana watakaoshiriki kozi hiyo chini ya Mkufunzi wa FIFA, Felix Tangawarima wa Zimbabwe ni 33 lakini Makocha watakaoshiriki kozi hiyo ni kutoka miokoa yote ya Tanzania ,mafunzo yatakayoongozwa na Mkufunzi Ulric Mathiott kutoka Shelisheli.


No comments:

Post a Comment