Thursday, 6 November 2014

SERIKALI IMEOMBA MSAADA WA FEDHA KUWASAIDIA WALIOKOSA MIKOPO ELIMU YA JUU


Serikali imeomba shilingi bilioni 3 wizara ya uchumi kwa lengo la kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu waliokosa mikopo.
 
waziri mkuu wa tanzania mheshimiwa Kayanza Peter Mizengo Pinda

Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema serikali imeomba shilingi bilioni 13 wizara ya fedha na uchumi ili iweze kuharakisha kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu zaidi ya elfu nane waliokosa mikopo baada ya serikali kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya sayansi.

Akijibu swali la Mbunge wa kigoma Kaskazini Mhe. Kabwe Zitto aliyetaka kujua serikali inachukua hatua gani kuhakikisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu zaidi ya elfu nane kukosa mikopo kutokana na serikali kukumbwa na changamoto ya kuwa na mahitaji makubwa zaidi kuliko fedha inazokusanya.
 
Akijibu swali la mbunge Rajabu Mbaruk Mohamed aliyetaka nini tamko la serikali baada ya wafadhili kusitisha kuisaidia tanzania, mheshimi pinda amesema wahisani wamekuwa na sababu tofauti ambapo kwa sasa wanadai wanangoja kuona taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali na iwapo wataikubali ndio wataweza kutoa hizo fedha jambo ambalo uamuzi huo unaenda kuathiri watu wengi badala ya watu wachache.
 
Aidha ameongeza kuwa kuwepo kwa taarifa za kupokea taarifa kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali Mhe.Pinda amesema Ofisi yake haijapokea taarifa hiyo na kuahidi kuifikisha taarifa hiyo bungeni punde kwa spika kama utaratibu unavyotaka.

No comments:

Post a Comment