Timu za Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zinazojiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinacheza Jumamosi ya Agosti 23 katika mechi ya majaribio ya mfumo mpya wa wa tiketi za elektroniki.
Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa 10 jioni wakati kiingilio kitakuwa sh. 1,000.
Tiketi za mechi hiyo zitaanza kuuzwa hapo kesho kupitia mtandao wa simu wa M-Pesa, benki za CRDB Simbanking na maduka 30 ya Fahari Huduma yaliyopo katika wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, wengi wao wakiwa Morogoro Mjini.
Washabiki 100 wa kwanza kuingia uwanjani watapata jezi bure za timu za Mtibwa Sugar na Polisi.
Tayari mechi ya majaribio ya tiketi za elektroniki
imeshafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo timu
za Tanzania Prisons na Mbeya City zilipambana na kutoka sare.
Mechi nyingine za majaribio ya tiketi za elektroniki zitachezwa Agosti 30 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini utakuwa na mechi kati ya Coastal Union na Mgambo Shooting wakati katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ni Kagera Sugar dhidi ya mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars.
Septemba 6 pia katika Uwanja wa Taifa kutakuwa na mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar. Mechi nyingine ni ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga itakayofanyika Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment