Tuesday, 19 August 2014

VIJANA 10 ARSENAL WAPATA SARE UGENINI LIGI YA MABINGWA

>>ni play off dhidi ya beskitas

>>Ramsey aondoka na kadi nyekundu 

ARSENAL imejiweka katika mazingira mazuri ya kuvuka hatua ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji Beskitas, Uwanja wa Ataturk. 
The Gunnes walimpoteza nyota wao, Aaron Ramsey aliyeonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu dakika ya 80 baada ya kucheza rafu.
mshambuliaji mpya wa Besiktas aliyejiunga kwa Pauni Milioni 4.7 kutoka Chelsea msimu huuakionesha vitu vyake.
Katika mchezo huo, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Demba Ba  alipiga shuti kali lililogonga besela la lango la arsenal mnamo dakika ya sita ya mchezo , wakati Alex Oxlade-Chamberlain naye akikosa kuifungia Arsenal pale alipogongesha mwamba mwishoni.
 
kwa matokeo haya arsenal watahitaji sare ya magoli yoyote au ushindi ili kusonga mbele.
 
Kocha wa Besiktas, Slaven Bilic pia alipandishwa jukwaani mwishoni mwa mchezo. Mchezo wa marudiano utafanyika Jumatano ijayo Uwanja wa Emirates. 
 
Kikosi cha Besiktas: Tolga, İsmail, Motta, Ersan, Pedro, Olcay/Tore dk72, Veli, Necip, Ozyakup/Frei dk80, Mustafa/Tosun dk88 na Demba Ba.
Arsenal: Szczesny, Debuchy, Koscielny, Chambers, Monreal, Arteta/Flamini dk50, Ramsey, Cazorla/Rosicky dk90, Wilshere, Sanchez/Oxlade-Chamberlain dk72 na Giroud.

No comments:

Post a Comment